Uromyces appendiculatus
Kuvu
Dalili za kwanza hujitokeza kama upele/malengelenge madogo sana ya kahawia hadi njano ambayo hupasua ngozi ya majani yaliyokomaa, hususani upande wa chini. Kadri muda unavyoenda, malengelenge haya yanaweza kuzungukwa na duara la mwanga wa tishu za manjano na yanaweza kugeuka na kuwa meusi zaidi. Malengelenge yalivyorefuka ya aina hiyo hiyo yanaweza kujitokeza kwenye vikonyo, mashina, na maganda. Majani yanaweza kubadilika rangi na kuwa ya njano na kukauka, na yanaweza kudondoka mapema. Kupukutika kwa majani kunaweza kutokea, na kuathiri mavuno. Kutu ya maharage inaweza kuua mimea michanga. Kwa mimea ya iliyokomaa, kuvu huwa na athari ndogo sana kwenye mavuno.
Dawa za kuua wadudu za kibaiolojia zinazotokana na spishi za Bacillus subtilis, Arthrobacter, na Streptomyces zina athari kubwa kwenye maendeleo ya ugonjwa huo.
Kila wakati zingatia mbinu jumuishi yenye hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaiyolojia. Dawa za kuvu za triazole na strobilurin zinaonyesha matokeo yenye matumaini katika kudhibiti kutu ya maharage.
Kuvu anayeitwa Uromyces appendiculatus huishi kwenye mabaki ya mimea kwenye udongo kipindi chote cha baridi. Ni kimelea tegemezi, ikiwa na maana kwamba kinahitaji tishu za mimea ili kiweze kuishi. Maambukizi ya awali hutokea wakati vijimbegu vya kuvu vinasambazwa kwenye mimea kupitia upepo, maji, na kupitia wadudu. Kuvu hii hustawi katika hali ya unyevunyevu wa juu na joto la juu. Vijimbegu vya kuvu vinaweza kusambaa kwa haraka sana katika hali hizi. Ugonjwa huwa mbaya zaidi wakati wa vipindi virefu vya hali ya hewa ya joto na unyevunyevu.