Colletotrichum lindemuthianum
Kuvu
Miche inayokua kutoka kwenye mbegu zilizoambukizwa mara nyingi huwa na madoa yaliyozama kwenye majani na mashina, yakiwa na rangi ya kahawia iliyokolea hadi nyeusi. Ukuaji wa miche hiyo huathiriwa na inaweza kufa mapema au kuonyesha ukuaji uliodumaa. Wakati wa maambukizi ya upili, mishipa ya majani na sehemu za vikonyo huonyesha madoa ya mstatili yenye rangi ya kahawia nyekundu, kwanza upande wa chini wa majani, kisha kwenye upande wa juu vile vile. Vidonda vya mviringo, vyenye rangi ya kahawia nyepesi hadi ya kutu, viliyovyuzungukwa na ukingo mweusi, huonekana kwenye maganda na mashina. Katika maganda yaliyoathiriwa vibaya, madoa haya yanaweza kukunjamana na kuwa na umbo lililoharibika kidogo, na kuwa na muonekano wa vikwachu vilivyozama. Mbegu zilizoambukizwa mara nyingi hubadilika rangi na kuonyesha vikwachu vya kahawia hadi vyeusi. Mimea ya maharage ya kawaida ni rahisi sana kushambuliwa na ugonjwa huu.
Mafuta ya mti wa mwarobaini yanayowekwa kila baada ya siku 7 hadi 10 wakati wa kipindi chenye joto zaidi cha msimu wa ukuaji hupunguza ukuaji wa kuvu. Tiba za kibaiolojia (matumizi ya wadudu na vijidudu) pia zinaweza kusaidia kudhibiti maambukizi. Tiba za udhibiti kibaiolojia kama vile kuvu Trichoderma harzianum na bakteria Pseudomonas fluorescens kwa mfano, hupunguza ukuaji wa Colletotrichum lindemuthianum ikiwa vitatumika kama matibabu ya mbegu. Zamisha mbegu kwenye maji moto (50°C) kwa dakika 10 ili kuua kuvu.
Daima fikiria kutumia mbinu jumuishi zikiwemo hatua za kinga pamoja na matibabu ya kibaiolojia yanayopatikana. Upuliziaji wa dawa za kuua kuvu kwenye majani unaweza kupunguza ukali wa ugonjwa shambani, lakini ni mara chache ndipo huwa na unafuu. Tumia dawa za kuua kuvu zenye mancozeb, chlorothalonil, flutriafol, penconazole, au bidhaa za madawa yanayotokana na shaba wakati majani yakiwa makavu.
Ugonjwa wa madoa meusi husababishwa na kuvu aitwaye Colletotrichum lindemuthianum. Ugonjwa huu huenezwa zaidi kwa njia ya mbegu, lakini pia huishi kwenye mabaki ya mazao na kwenye mazao mbadala yanayohifadhi ugonjwa huu. Wakati hali za kimazingira zinapokuwa rafiki, kuvu hii hutoa vijimbegu vyake na huenezwa shambani kwa njia ya upepo na mvua. Joto la wastani hadi ubaridi (13-21°C), vipindi vya unyevunyevu wa juu, umande, majani yenye unyevunyevu au mvua za mara kwa mara vyote hivyo huchochea mzunguko wa maisha ya kuvu na mwendelezo wa ugonjwa huu. Kwa kuwa kuvu hii huenezwa kwa uwepo wa maji, inaweza pia kuenea kutokana na majeraha ya mimea wakati wa kazi za shambani zinapofanywa wakati majani yakiwa na unyevunyevu. Kuvu hii inaweza kushambulia maganda na kuambukiza kotiledoni au ngozi ya mbegu.