Verticillium spp.
Kuvu
Dalili zinatofautiana sana kati ya mazao tofauti. Kwa kawaida, manjano hutokea kwanza kwenye kingo za majani ya zamani. Kadri rangi ya manjano inavyoenea kwenye sehemu nyingine za tishu, jani linachukua muonekano wa kunyauka, mara nyingi upande mmoja tu. Sifa hii maalum inaitwa umanjano wa upande au "unyaukaji wa upande mmoja." Madoa meusi hujitokeza kwenye shina na kuenea kutoka chini kuelekea juu, na kusababisha kunyauka kwa shina. Dalili kuu kwenye miti, ni ukuaji duni, majani kukauka mapema, kudumaa, na kufa kwa matawi yote. Dalili za ziada ni kuchafua tishu za miti kwa njia ya miduara au michirizi. Wakati mwingine, kwa uchunguzi wa karibu kwa kutumia lenzi, madoa meusi madogo yanaweza kuonekana kwenye tishu zinazokufa au kwenye tishu hai vile vile.
Dawa za kibaiolojia za kudhibiti kuvu wenye Streptomyces lydicus huvunja mzunguko wa maisha wa kuvu na zinaweza kusaidia kudhibiti maendeleo ya ugonjwa.
Daima zingatia mbinu jumuishi zikiwa na hatua za kukinga pamoja na tiba za kibaiolojia ikiwa zinapatikana. Ikiwa mimea imeathirika na ugonjwa huu, inakuwa vigumu sana kuutokomeza. Matumizi ya dawa za kudhibiti wadudu waharibifu kwenye udongo ni mbinu yenye ufanisi lakini ni yenye gharama. Ufanisi wake unategemea kemikali iliyotumika, kiwango chake, na hali ya mazingira wakati wa ilipotumika kemikali husika. Tiba ya sehemu za mimea zilizoathirika pia inaweza kuzingatiwa.
Dalili hizi husababishwa na kuvu/ukungu wanaoishi kwenye udongo, na miongoni mwao ni pamoja na V. dahliae, ambao wanaweza kuishi kwenye mabaki ya mazao kwenye udongo inapokuwa hakuna mimea mbadala ambayo kuvu wanaweza kuishi. Kuvu huingia kwenye tishu za mishipa ya mmea kupitia mizizi midogo au majeraha kwenye gome. Mara wanapokuwa ndani ya mmea au mti, kuvu hukua haraka na kuzuia usafirishaji wa maji na virutubisho, na kusababisha kunyauka na kuoza kwa sehemu za juu (majani na mashina). Hali hii huongezeka zaidi wakati wa hali ya hewa ya joto na jua kali. Katika hatua za baadaye za ugonjwa, kuvu huenea kwenye tishu zinazokufa na kutengeneza miundo ya giza inayoweza kuonekana kwa lenzi ya kukuza. Kuvu hawa wanaweza kuishi kwa miaka kadhaa kwenye eneo husika.