Tranzschelia pruni spinosae
Kuvu
Ugonjwa huu huathiri miti jamii ya mizambarau na mara chache miti mingine ya matunda jamii ya fyulisi (peaches). Dalili huonekana kuanzia mwishoni mwa majira ya kuchipua kwenye majani na zinaweza kutofautiana kidogo kulingana na aina za miti. Mwanzoni, madoa madogo, yaliyo chongoka, yenye rangi ya njano iliyokolea huunda muonekano wa nakshi kwenye uso wa juu wa jani. Ugonjwa unapoendelea, upele/ukurutu wenye kutu hadi rangi ya kahawia nyepesi huonekana chini ya madoa haya kwenye sehemu ya chini ya jani. Baadaye katika msimu, hugeuka na kuwa na rangi ya kahawia iliyokolea au nyeusi. Majani yaliyoathirika sana hukauka, hugeuka kahawia na kuanguka haraka sana. Upukutishaji mapema wa majani kabla hayaja komaa unaweza kuathiri ukuaji wa maua na ubora wa matunda katika misimu inayofuata. Zaidi ya hayo, ikiwa utaendelea kwenye mti huo huo mwaka baada ya mwaka, unaweza kudhoofisha nguvu ya mti. Matunda yanaweza kuwa na dosari na kwa hivyo yanakosa soko.
Kawaida, matibabu sio lazima kwani kuvu hawa huonekana bila mpangilio, hawadhoofishi mti na hawaathiri moja kwa moja matunda.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Unyunyiziaji wa dawa za kuua kuvu unapaswa kuanza mara moja baada ya dalili za kwanza za maambukizi kuonekana. Matumizi yaa bidhaa zitokanazo na myclobutanil, pyraclostrobin, boscalid, mancozeb, trifloxystrobin au difenoconazole yanaweza kusaidia kudhibiti ugonjwa huo. Katika hali ya maambukizi ya baadae/kuchelewa, matibabu yanapaswa kufanyika moja kwa moja baada ya mavuno, ikiwa inawezekana.
Dalili husababishwa na fangasi Tranzschelia pruni-spinosae, ambao ni vimelea tegemezi, kumaanisha kwamba wanahitaji tishu hai ili kukamilisha mzunguko wake wa maisha. Kuvu hawa wanaweza kusalia msimu mzima wa baridi kali kama vijimbegu vilivyo wekwa kwenye mianya ya magome ya matawi au kwenye magamba ya machipukizi. Vinginevyo, hubadilisha wenyeji/mimea mwishoni mwa msimu wa kiangazi na kuishi kwenye mimea jamii ya Anemone wakati miti ya jamii ya mizambarau inapokuwa bwete(dormant). Madoa kwenye sehemu ya chini ya majani yana miundo inayozalisha vijimbegu ambayo hutoa aina mbili za vijimbegu: moja ambayo huambukiza matunda jamii ya fyulisi wakati wa masika na majira ya kiangazi au inayoambukiza mimea mbadala mwishoni mwa msimu. Katika hali zote mbili, vijimbegu huota kwa urahisi ikiwa kuna unyevu kwenye majani (umande au mvua). Mwinuko mdogo, maeneo yenye unyevunyevu na aina zinazo athiriwa kirahisi huwezesha kutokea kwa kuvu. Ugonjwa umeonekana katika sehemu nyingi za ulimwengu. Unaenea kwa haraka na unaweza kuchukua uwiano wa magonjwa ya mlipuko ikiwa hali ya hewa ni nzuri kwa ukuaji wake.