Wilsonomyces carpophilus
Kuvu
Dalili za awali huonekana wakati wa majira ya kuchipua na zinajulikana kwa uundwaji wa madoa ya rangi ya zambarau au nyekundu kwenye majani mapya, na wakati mwingine kwenye mashina na vichipukizi. Mara nyingi madoa haya huzungukwa na ukingo wa kijani nyepesi au manjano. Madoa haya yanapopanuka, katikati yake hubadilika rangi na kuwa ya kahawia au rangi ya kutu na mwishowe hudondoka, na kuacha sifa ya 'shimo la risasi' kwenye matawi ambako ugonjwa hutoa jina lake. Udondokaji majani mapema unaweza kutokea. Vitawi vichanga vinaweza kutoa machipukizi yaliyokufa, vidonda au vikwachu vinavyotoa ulimbo. Kwenye matunda, hutokea vidonda mparuzo na mithili ya magamba yakiwa na kingo za rangi ya zambarau, kwa ujumla upande wa juu tu. Hali hii hufanya tunda lisivutie na kutouzika. Vidoa vidogo vyeusi vinaweza kuonekana kwa kutumia lensi ya kukuza katikati ya vidonda.
Kunyunyizia dawa ya kuua ukungu (fangasi) inayotokana na shaba mwanzoni mwa majira ya baridi inaweza kuwa ulinzi wa kwanza dhidi ya ugonjwa huo. Mchanganyiko wa Bordeaux unaotengenezwa nyumbani au utengenezaji wa kibiashara wa shaba unaweza kununuliwa. Salfate ya zinki inaweza kunyunyiziwa kwenye majani mwishoni mwa majira ya Vuli ili kuharakisha udondokaji wa majani na kupunguza uwepo wa Kuvu kabla ya kuanza kwa msimu mpya.
Wakati wote zingatia mbinu jumuishi zikiwa na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Ili kulinda matunda, dawa za kuua ukungu (kuvu) zinaweza kunyunyiziwa kabla na baada ya kipindi cha maua, kuanzia kwenye utokaji wa vichipukizi hadi kuanguka kwa petali. Takwimu za hali ya hewa wakati wa kutoka maua itaonyesha ikiwa dawa zinahitajika kulinda matunda au la. Kwa kuwa matumizi ya shaba hayapendekezwi tena katika hatua hii, dawa za kuua kuvu zinazotokana na thiram, ziram, azoxystrobin, chlorothalonil, iprodione ndizo zinapendekezwa.
Dalili husababishwa na Kuvu Wilsonomyces carpophilus, ambayo huambukiza aina kadhaa za matunda ya mawe [mafyulisi (mapichi), lozi, cheri na aprikoti). Mimea mingine inayobeba ugonjwa huu ni pamoja na ni laurusi ya Kiingereza (mmea aina ya mdalasini) na nektarini. Kuvu huishi kipindi chote cha baridi kwenye vidonda vya kwenye vichipukizi na matawi au katika matunda yaliyokaushwa. Wakati hali ya hewa ni nzuri, huanza ukuaji na kutoa viiniyoga (vijimbegu) ambavyo hutawanywa na mvua hadi kwenye tishu zenye afya. Kipindi kirefu cha unyevunyevu wa majani (saa 14-24 au zaidi) na halijoto ya takribani 22 °C huwezesha mzunguko wa maisha wa Kuvu na uwezekano wake wa kuambukiza miti yenye afya. Majira ya joto, ukungu, au mvua za majira ya baridi pamoja na mvua kubwa za mwishoni, hizo ni hali zinazowezesha utengenezaji na kutolewa kwa vijimbegu. Hakika ugonjwa huo utakua kwenye miti ya matunda ya mawe tu wakati wa hali ya hewa isiyo ya kawaida ya unyevu wakati wa majira ya kuchipua.