Mpichi

Ugonjwa wa Kujikunja kwa Majani ya Fyulisi

Taphrina deformans

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Uharibifu wa umbile la majani na kubadilika rangi kuwa na wekundu.
  • Ukuaji wa kuvu kwenye majani.
  • Kupukutika kwa majani mapema.

Inaweza pia kupatikana kwenye

3 Mazao
Mlozi
Aprikoti
Mpichi

Mpichi

Dalili

Dalili kawaida huonekana mara tu baada ya jani kupasuka. Majani yanakuwa manene na umbile lililo haribika sana na kiungo kilichojikunja, yaliyokunjamana na kubadilika rangi kutoka nyekundu hadi zambarau, kulingana na aina ya mti. Maambukizi yanapoendelea, majani yaliyoathiriwa huchukua mwonekano mweupe-kijivu, mwonekano wa unga unga/poda kwa sababu ya kuchipua kwa kuvu kwenye uso wa majani. Utando wa kijivu hatua kwa hatua hugeuka kuwa mweusi, mchakato unaoendanana joto la juu la mchana. Hatimaye, majani yenye ugonjwa hufa na kuanguka, na kusababisha upukutishaji wa majani na kupoteza afya. Mapema hubadilishwa na majani mapya yanayotokea kwenye sehemu sawa na ya ukuaji. Maeneo ya gome au chipukizi zima yanaweza pia kuwa meusi wakati maambukizi yanapokuwa ya ndani, wakati ambapo kuvu wataanza kuenea ndani ya tishu za ndani za mmea. Katika matukio hayo, ncha zinazokua huzalisha machipukizi ya pembeni/ulalo yasiyo ya kawaida na kuleta mwonekano wa mifagio ya mchawi. Juu ya miti iliyoathiriwa sana na ugonjwa, sura ya matunda huonyesha mabadiliko makubwa katika muonekano.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Dawa za kuua kuvu zilizo na misombo ya asili ya shaba kama mchanganyiko wa Bordeaux zinaweza kutumika kupambana na kuvu hawa. Matibabu ya kwanza yanapaswa kufanyika baada ya pukutiko katika msimu wa vuli na kurudiwa katika msimu wa kuchipua kabla ya machipukizi kuanza kuvimba. Kumbuka kwamba matumizi ya mara kwa mara ya bidhaa za shaba yanaweza kusababisha mkusanyiko wa shaba kwenye udongo, ambayo hatimaye yanaweza kuwa sumu kwa viumbe wa kwenye udongo.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia, ikiwa yanapatikana. Dawa za kuua kuvu zenye copper oxychloride, cupric hydroxide, thiram, ziram, chlorothalonil au difenoconazole zinaweza kutumika. Matibabu ya kwanza yanapaswa kufanyika baada ya pukutiko katika msimu wa vuli na kurudiwa katika msimu wa kuchipua kabla ya machipukizi kuanza kuvimba.

Ni nini kilisababisha?

Dalili husababishwa na kuvu Taphrina deformans kukalia/kutawala tishu za mmea. Vijimbegu vinavyo zalishwa kwenye uso wa jani huoshwa na matone ya mvua au kupeperushwa na upepo kwenye matawi ya mti wa fyulisi na machipukizi, kuanzisha maambukizi mapya. Vijimbegu huota wakati wa mvua za mara kwa mara wakati machipukizi yanapofunguka katika majira ya kuchipua na kuambukiza majani ambayo bado hayajafunguka. Tangu vijimbegu vinapoingia kwenye chipukizi la jani, hakuna hatua madhubuti ya kuzuia mchakato wa kuambukiza. Ikiwa mvua haitokei wakati huu, vijimbegu hubakia tuli bila kufanya kazi na maambukizi kidogo au hakuna kabisa. Vikiwa kwenye magamba ya chipukizi au mianya ya gome wakati wote wa kiangazi na majira ya baridi kali, hatimaye huota wakati wa msimu unaofuata. Kuvu hawa huwa amilifu katika joto la hadi 16 ° C na wanaweza kuzaliana tu kwa joto hili la chini. Taphrina deformans huambukiza mafayulisi na matunda mengine ya jamii hiyo, pia mlozi na mara chache aprikoti na mimea ya mapambo jamii ya Prunus.


Hatua za Kuzuia

  • Kinga mimea na mvua au umwagiliaji wa juu wakati wa awamu ya utokeaji wa machipukizi.
  • Pogoa mwavuli/taji la mti kila mwaka ili kuruhusu uingizaji hewa mzuri kwenye majani.
  • Tumia kiasi cha wastani cha mbolea.
  • Tumia virutubisho vya mimea kabla ya kutokea machipukizi.
  • Panda aina zinazostahimili, kwa mfano, aina za nyama nyeupe.
  • Ondoa na uharibu majani yote ambayo yameambukizwa, matunda yaliyo kauka na machipukizi.
  • Inapowezekana, tumia vizuizi vya mvua vya plastiki kuzuia maambukizi.

Pakua Plantix