Pea

Kutu Ulaya ya Peasi

Gymnosporangium sabinae

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Rangi ya machungwa-nyekundu inayong`aa, madoa ya duara yanaonekana kwenye uso wa juu wa majani.
  • Vijidudu vya rangi ya kahawia vyenye umbo kama la nyongo hukua kwenye sehemu za chini za majani.
  • Mara chache, vidonda vilivyo chimbika kwenye magome ya matawi na mashina machanga.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao
Pea

Pea

Dalili

Madoa madogo ya duara, yenye rangi ya kahawia hukua kwanza kwenye sehemu ya juu ya majani. Yanapo tanuka, hubadilika na kuwa na rangi ya machungwa-nyekundu inayo ng`aa na katikati huwa na rangi ya hudhurungi nyeusi. Mwishoni mwa majira ya joto, vijidudu vyenye umbile la punje ya nafaka,vijiotea vyenye umbo la nyongo na rangi ya kahawia huonekana upande wa chini wa majani. Mara chache, kuvu huweza pia kusababisha vidonda na majeraha yaliyo chimbika katika magome ya matawi na mashina machanga. Ingawa matunda hayaathiriwi moja kwa moja, maambukizi makali yanaweza kusababisha kupukutika kwa majani na upotevu wa mazao.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Hadi leo, hakuna matibabu ya kibayolojia yanayojulikana kwa ajili ya ugonjwa huu.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Viwango vya chini vya maambukizi kawaida havina shida na vinaweza kupuuzwa tu. Dawa za kuua kuvu zenye difenoconazole zinaweza kutumika kudhibiti ugonjwa huu. Kwa wenye bustani za nyumbani, dawa za kuua kuvu tebuconazole, tebuconazole na trifloxystrobin, na triticonazole zimeidhinishwa kudhibiti magonjwa ya kutu.

Ni nini kilisababisha?

Dalili husababishwa na kuvu aina ya Gymnosporangium sabinae, ambao hushambulia miti ya peasi na mireteni. Peasi ni mwenyeji wa kati tu wa vimelea na miti yote miwili inahitajika kukamilisha mzunguko wake wa maisha. Kuvu hao hawawezi kuishi kwenye sehemu/mabaki ya mimea iliyokufa, kwa hivyo ni lazima wabadilishe mwenyeji. Kuvu hujificha kwenye mireteni, ambayo ndio mwenyeji wake mkuu. Katika majira ya kuchipua, vijimbegu huenea kutoka kwenye mireteni na kuambukiza miti ya peasi iliyo karibu. Madoa yanayotokea upande wa chini wa majani ya peasi kiuhalisia huwa ni miundo inayozalisha vijimbegu/chavua. Chavua hizo haziwezi kuathiri tena majani ya peasi, kwa hivyo mwishoni mwa msimu wa joto/kiangazi, hutawanywa kwa umbali mrefu (hadi mita 500) ili kuambukiza mireteni mipya. Huko, husababisha uvimbe wa kudumu wenye umbo kama la pembe kwenye matawi. Uvimbe huo huonekana hasa katika majira ya kuchipua/mvua, kufuatia vipindi vya unyevu mwingi.


Hatua za Kuzuia

  • Punguza kwa uangalifu maumbile ya kuvu kwenye mipeasi.
  • Vinginevyo, ondoa miti iliyo karibu iliyosimama.
  • Ongeza virutubisho vya mimea ili kuimarisha miti yako ya peasi.
  • Kata tawi lolote lililoambukizwa linaloonekana kwenye peasi, sio jani moja moja.

Pakua Plantix