Venturia inaequalis
Kuvu
Dalili za kwanza zinazoonekana za upele wa tufaha huonekana wakati wa majira ya kuchipua zikiwa ni madoa madogo, mviringo, na yenye rangi ya kijani iliyopauka kwenye majani, na mara nyingi kwenye kishipajani kikuu. Kadri madoa yanapokua, yanageuka na kuwa yenye rangi ya kahawia-nyeusi na hatimaye kuungana na kutengeneza mabaka makubwa yenye tishu zilizokufa. Majani yaliyoathiriwa mara nyingi huharibika na kudondoka kabla ya wakati, na hivyo kusababisha kupukutika kwa majani ikiwa kuna maambukizi makubwa. Kwenye vichipukizi, maambukizi husababisha malengelenge na mipasuko ambayo inaweza kuruhusu viini vya magonjwa nyemelezi. Kwenye matunda, maduara yenye rangi ya kahawia hadi kahawia nyeusi huonekana kwenye matunda. Kadri yanapokua zaidi, mara nyingi maduara haya huungana na kuanza kuongezeka ukubwa, kuwa magumu na kuwa gamba. Hii inazuia ukuaji wa matunda na husababisha kuharibika na kupasuka kwa ngozi na hivyo kuacha tunda likiwa wazi. Mashambulizi mepesi hayaathiri ubora wa matunda kwa kiasi kikubwa. Hata hivyo, upele unaweza kuhatarisha matunda dhidi ya vimelea vya magonjwa nyemelezi na kuoza, na hivyo kupunguza uwezo wa kuhifadhi na ubora.
Endapo viwango vya ugonjwa vilikuwa vya juu msimu uliopita, viua kuvu vya shaba vya maji maji vinaweza kunyunyiziwa ili kuzuia ukuaji wa ukungu kwenye mti wakati wa msimu wa baridi. Vinyunyuzi vya salfa vinafaa kwa sehemu tu dhidi ya kigaga cha tufaha. Hata hivyo, suluhu zenye salfa na pyrethrin zinapatikana kwa udhibiti wa kikaboni wa ugonjwa wakati wa msimu wa ukuaji.
Wakati wote zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Dawa za kuua kuvu kama vile dodine, captan au dinathion zinaweza kunyunyiziwa sehemu zilizovunika za vichipukizi ili kuzuia ugonjwa huo. Mara tu kigaga auupele unapogundulika, dawa za kuua kuvu zinazotokana na difenoconazole, myclobutanil au salfa zinaweza kutumika kudhibiti ukuaji wa kuvu. Hakikisha matumizi ya madawa za kuua ukungu zinatokana na makundi tofauti ya kemikali ili kutofanya magonjwa kuwa sugu na madawa.
Upele wa tufaha ni ugonjwa unaosababishwa na kuvu au ukungu anayeitwa Venturia inaequalis. Kuvu hawa wanastahimili majira ya baridi hususani kwenye majani yaliyoambukizwa yaliyopo ardhini lakini pia kwenye magamba ya vichipukizi au vidonda kwenye mti. Mwanzoni mwa majira ya kuchipua, kuvu (ukungu) huanza tena ukuaji na huanza kutoa vijimbegu(vijidudu), ambavyyo baadaye hutoka na kutawanywa umbali mrefu na upepo. Vijimbegu au vijidudu hivi hutua kwenye majani na matunda yanayokua na kuanzisha maambukizi mapya. Sehemu za nje za vichipukizi ambavyo havijafunguka huathirika kirahisi sana na upele. Hata hivyo, matunda yanapokomaa, kiwango cha kuathirika hupungua. Mazingira yenye unyevunyevu, kipindi cha unyevu wa majani au matunda ni muhimu kwa maambukizi. Mimea au vitu mbadala vinavyoweza kubeba vimelea vya magonjwa ni pamoja na vichaka vya nasaba ya Cotoneaster (yaani mimea inayotoa maua ya jamii ya waridi), Pyracantha (vichaka vyenye miba), na Sorbus. Aina zote za tufaha hushambuliwa na upele (kigaga), huku matufaha aina ya Gala yakiwa katika hatari zaidi ya kupata maambukizi.