Mtama

Ubwiri Vinyoya

Sclerospora graminicola

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Sehemu za maua zinaonyesha maumbile kama ya majani.
  • Ukuaji wa kuvu (ukungu) kwenye upande wa chini wa majani.
  • Madoa ya manjano kwenye majani.
  • Hakuna uzalishaji wa vishada vya maua.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Mtama

Dalili

Kitako cha jani kinakuwa na rangi ya manjano. Sehemu za maua zinaonyesha maumbile kama ya majani na zinaweza pia kuwa na rangi iliyofifia. Katika hali mbaya, mmea hudumaa na hauzalishi vishada vya maua.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Tibu mbegu zako kwa kutumia Pseudomonas fluorescens na baadae ipulizie kwenye miche. Vichochezi vya kibaiolojia kama Trichoderma harzianum (20 g kwa kila kilo 1 ya mbegu), Pseudomonas fluorescens, na aina za Bacillus (10 g kwa kila kilo 1 ya mbegu) vile vile husaidia kudhibiti ugonjwa kama matibabu ya mbegu.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na zenye hatua za kukinga pamoja na matibabu ya kibaiolojia, ikiwa yanapatikana. Ili kuzuia maambukizi kupitia mbegu, unapaswa kutibu mbegu kwa dawa za kuua kuvu kama captan, fludioxonil, metalaxyl au thiram. Metalaxyl pia inaweza kutumika kudhibiti ubwiri vinyoya moja kwa moja.

Ni nini kilisababisha?

Dalili hizi husababishwa na kuvu Sclerospora graminicola na zinaweza kutofautiana sana kutegemea na mimea mbadala inayohifadhi vimelea vya magonjwa, hali za mazingira, na muda wa ugonjwa. Ugonjwa huu pia unajulikana kama Ugonjwa wa Sikio la Kijani, kwa sababu sehemu za maua za mmea hubadilishwa na kuwa na umbile/umbo mithili ya majani. Vijimbegu vya Ubwiri Vinyoya huishi kwenye udongo, mabaki ya mazao yaliyoathirika, na kwenye mbegu. Vijimbegu vya kuvu vinasafirishwa kwenye udongo kwa njia ya maji na juu ya ardhi kwa njia ya upepo na maji.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia mbegu zisizo na magonjwa.
  • Panda aina ya mbegu zilizo sugu dhidi ya magonjwa.
  • Tibu mbegu mara kwa mara kwa kutumia dawa ya kuua kuvu.
  • Tumia samadi inayotokana na takataka za wanyama wanaofugwa na binadamu kwa kiwango cha tani 5 kwa hekta ikichanganywa na udongo kwenye mashimo ya mbegu.
  • Ondoa mimea iliyoathirika mara moja.
  • Baada ya mavuno, angamiza mabaki ya mimea ama kwa kuyachoma moto au kuyakatua.

Pakua Plantix