Saladi

Ubwiri Vinyoya

Peronosporales

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Madoa ya manjano kwenye majani - baadaye mabaka ya kahawia yaliyokufa.
  • Tabaka jeupe hadi kijivu lililo mithili ya pamba kwenye upande wa chini wa jani.
  • Kupukutika kwa majani.
  • Ukuaji uliodumaa.
  • Machipukizi machanga, maua, na matunda hufa.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Saladi

Dalili

Madoa ya manjano yenye ukubwa tofauti huonekana kwenye uso wa majani yanayokua. Baadaye madoa huongezeka ukubwa na kuwa na pembe kali na kuzingirwa na vishipajani. Katikati yake huanza kuwa na vivuli mbalimbali vya kahawia kutokana na kufa kwa tishu. Tabaka zito mithili ya pamba nyeupe hadi kijivu hutokea chini ya madoa baada ya mfululizo wa usiku wenye joto na unyevunyevu, na kutoweka mara tu kunapokuwa na jua. Machipukizi machanga hupukutika majani au hukutana na ukuaji uliodumaa. Ugonjwa pia huathiri matunda na sehemu nyingine za mimea.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Tiba za kibaolojia za kibiashara za kupambana na ukungu/kuvu zinapatikana. Katika hali ya wastani, mara nyingi ni bora kutofanya chochote na kusubiri hadi hali ya hewa inapokuwa nzuri. Katika baadhi ya matukio, dawa za kikaboni kabla ya kuambukizwa zinaweza kusaidia kuzuia uchafuzi wa mimea. Hizi ni pamoja na dawa za ukungu zinazotokana na shaba, kama vile mchanganyiko wa Bordeaux.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa inapatikana. Dawa za kuzuia kuvu/ukungu zinaweza kusaidia kuzuia uchafuzi wa mimea lakini zinapaswa kunyunyiziwa vizuri chini ya majani. Dawa za kuua kuvu za familia ya dithiocarbamates zinaweza kutumika. Dawa ya kuvu baada ya maambukizi lazima itumike mara tu baada ya kugundua dalili za kwanza. Dawa za kuua kuvu zinazotumika sana baada ya kuambukizwa ni pamoja na fosetyl-alumini, azoxystrobin na phenylamides (mfano metalaxyl-M).

Ni nini kilisababisha?

Dalili hizi zinasababishwa na kuvu aliye katika kundi la Peronosporales na anaweza kuwa na uharibifu mkubwa katika maeneo yenye vivuli na mvua za mara kwa mara na joto la wastani (15-23°C). Kuvu hawa wamejizoeza vizuri kwenye mimea yao inayowahifadhi, ikiwa na maana kwamba kila mazao makubwa huhifadhi spishi yake ya kuvu/ukungu. Katika kipindi chote cha baridi, kuvu huishi katika mabaki ya mimea iliyoambukizwa au machipukizi, katika udongo au kwenye mimea mbadala (mazao na magugu) inayohifadhi vimelea vya kuvu hao. Upepo na mvua husambaza vijimbegu vya kuvu wakati wa hali nzuri. Vijimbegu humea/huchipua na kuzalisha maumbo ambayo huingia kwenye jani kupitia vinyweleo/vitundu vya asili vilivyopo upande wa chini wa majani. Huko huanza kusambaa kupitia tishu, hatimaye kuzizidi tishu za ndani na kutengeneza tabaka jeupe kwa nje.


Hatua za Kuzuia

  • Chagua aina za mimea inayovumilia magonjwa, ikiwa inapatikana.
  • Hakikisha mimea inakuwa mikavu, kwa mfano kupitia mfumo mzuri wa uingizaji hewa.
  • Hakikisha kuna utiririshaji mzuri wa maji kwenye udongo.
  • Hakikisha utumiaji wa mbolea wenye uwiano sahihi kwa ajili ya uimara wa mimea.
  • Panda kwa kuacha nafasi nzuri kati ya mimea.
  • Panda katika maeneo yanayopata jua vizuri na chagua mwelekeo sahihi.
  • Dhibiti magugu shambani na kuzunguka shamba.
  • Ondoa mabaki ya mimea kutoka shambani.
  • Weka zana na vifaa vya kilimo katika hali ya usafi.
  • Epuka kusambaza udongo ulioambukizwa na vifaa vya mimea.
  • Virutubisho vinaweza kutumika ili kuimarisha afya ya mmea.

Pakua Plantix