Erysiphaceae
Kuvu
Kwa kawaida maambukizi huanza kama madoa ya duara, mithili ya unga mweupe ambayo yanaweza kuathiri majani, mashina na wakati mwingine matunda. Kwa kawaida hufunika sehemu za juu za majani lakini yanaweza kukua kwenye upande wa chini vile vile. Kuvu au ukungu huzuia usanisinuru (yaani uwezo wa mmea kutumia chakula na mwanga wa jua) na kusababisha Majani kugeuka na kuwa manjano na kukauka na baadhi ya majani yanaweza kujipinda, kuvunjika au kuharibika umbo lake. Katika hatua za baadaye, vichipuzi na ncha zinazokua huharibika maumbo yake.
Vinyunyuzi vya majani vinavyotokana na salfa, mafuta ya mwarobaini, kaolini au tindikali (asidi) askobiki vinaweza kuzuia maambukizi makali.
Wakati wote zingatia mbinu jumuishi na hatua za kinga pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Kwa kuzingatia idadi ya mazao ambayo huathirika na uburi unga, ni vigumu kupendekeza matibabu yoyote ya kemikali. Dawa za kuua kuvu zinazotokana na salfa yenye unyevunyevu (3 g/l), hexaconazole, myclobutanil (zote 2 ml/l) zinaonekana kudhibiti ukuaji wa kuvu katika baadhi ya mazao.
Chavua za kuvu huishi ndani ya vichipuzi vya majani na mabaki mengine ya mazao wakati wote wa majira ya baridi. Upepo, maji, na wadudu husambaza vijimbegu vya magonjwa kwenye mimea iliyo karibu. Ingawaje ni Kuvu, ukungu wa unga unaweza kukua kwa kawaida katika hali kavu. Inastahimili kwenye joto la kati ya 10-12 ° C, lakini hali bora hupatikana kwa 30 ° C. Tofauti na ubwiru unyoya, kiasi kidogo cha mvua na umande wa kawaida wa asubuhi huharakisha kuenea kwa uburi unga.