Matunzo
Zabibu ni tunda ambalo hukua kwenye spishi ya miti migumu itokayo kwenye familia ya Vitis. Kuna aina nyingi za zabibu ulimwenguni na zinaweza kuliwa au kutumika kutengenezea bidhaa nyingi tofauti tofauti ikiwa ni pamoja na divai, jeli, jamu, juisi, siki, zabibu kavu, mafuta ya zabibu, pamoja na kiziduo cha mbegu za zabibu. Zabibu zimekuwa zikilimwa na wanadamu kwa maelfu ya miaka na sasa zinapandwa na kufurahiwa duniani kote.
Udongo
Zabibu zinaweza kustahimili aina mbalimbali za udongo lakini aina bora zaidi ya udongo ni mchanga wa tifutifu wenye rutuba. Zabibu huhitaji kiasi cha wastani cha rutuba kwenye udongo. Kuongeza nitrojeni na potasiamu kwenye udongo kabla ya msimu wa ukuaji kunaweza kuwa na manufaa katika udongo wenye viwango vya chini vya virutubishi. Zabibu hukua vyema katika hali ya asidi kidogo yenye kiwango cha pH kuanzia 5.5-7.0. Udongo unaopitisha maji kiurahisi ni muhimu pia katika uzalishaji wa mizizi na katika kuzuia magonjwa ya mazao.
Hali ya hewa
Zabibu huota vyema katika hali ya hewa yenye majira ya baridi kali na kipindi kirefu cha vuguvugu wakati wa ukuaji. Zabibu huhitaji karibia mm 710 za mvua kila mwaka. Mvua nyingi sana au kidogo sana inaweza kusababisha madhara kwenye uzalishaji wa matunda. Mikoa ya Mediterania imefanikiwa sana katika uzalishaji wao wa zabibu kutokana na uwepo wa msimu tulivu wa ukuaji unaohusisha halijoto vuguvugu na kavu. Mizabibu inahitaji halijoto ya angalau nyuzi joto 10 za Selisiasi au nyuzi joto 50 za Farenhaiti ili kuanza hatua za kifiziolojia. Halijoto, mvua, pamoja na vichochezi vingine vya hali ya hewa wakati wa uzalishaji huathiri ladha ya zabibu. Hili huonekana hususan katika tasnia ya mvinyo ambapo tofauti ya tabia nchi ya kikanda huathiri ladha ya bidhaa ya mwisho. Zaidi ya hayo, aina fulani za zabibu hustawi zaidi kwenye maeneo na hali ya hewa maalum.